Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Tanzania kwa kushirikiana na serikali na wadau wake wameandaa mpango wa miaka mitano wenye lengo la kuoanisha shughuli za kilimo na lishe ili kukabiliana na utapiamlo.

Afisa lishe wa FAO Tanzania Stella Kimambo amesema wamepitia mpango jumuishi wa lishe na mpango wa maendeleo ya kilimo ASDPII, na kuangalia kasoro zilizopo na kuandaa mpango wa utekelezaji ili kuhamasisha mazao lishe.

Aidha, Kimambo amesisitiza wakulima kutokuuza mazao lishe yote wanayolima bali kubakiza ya kula katika familia na kuboresha lishe kwa njia ya chakula.

Kimambo amesema mwaka 2021 wataleta pamoja maafisa kilimo na wale wa lishe ili kuwajengea uwezo huku Afisa Kilimo Magret Natai akibainisha kuwa huo ni mpango wa kwanza ulioandaliwa kutekeleza lishe katika kilimo.

TRA yawaonya wasiotumia stempu za kielektroniki
Eng. Hersi aandika waraka mzito Young Africans