Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai anatarajiwa kutangaza kamati za Bunge muda wowote.

Duru kutoka ndani ya ofisi za Bunge zimeeleza kuwa Spika wa Bunge ameendelea kukamilisha mchakato huo na kwamba muda wowote ndani ya wiki hii kamati hizo zitajulikana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha Bunge hilo, Januari 26 mwaka huu.

“Spika anashughulikia suala la kamati naamini hivi karibuni zitakuwa zimekamilika na kutangazwa hadharani hata kabla ya kuanza kwa Bunge lijalo,” Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Bunge, Owen Mwandumbya alimwambia mwandishi wa Mtanzania.

Jamal Malinzi Aungana Na Familia Ya Juma Ally Khamis
Samuel Eto'o Avuliwa Kofia Ya Ukocha