Huko Berlin, Ujerumani Waziri wa mambo ya nje, Sigmar Gabriel ameungana na Urusi, Iran na China kulaani mipango ya Serikali ya Rais wa Marekani Donald Trump, kuboresha kiwango cha silaha za nyuklia.
Gabriel amesema umefika wakati Umoja wa Ulaya (EU) kuongeza shinikizo la kuwapo dunia isiyo na silaha za nyuklia.
Kauli hiyo ameitoa kujibu tathmini ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani kuhusu tishio la nyuklia katika miongo ijayo.
Mpango huo uliotangazwa Ijumaa iliyopita unamaanisha wazi mkakati mpya wa utawala wa Trump wa kijeshi na nyuklia.
-
Aliyesimamia kuapishwa kwa Raila ashtakiwa kwa uhaini
-
Aliyemuua Bob Marley ajitokeza, adai kutekeleza mpango wa Marekani kuwaua…
Wizara hiyo ya ulinzi pia imezitaja Urusi na China kama tishio kubwa linaloikabili Marekani.
Wakati Ujerumani yenyewe haina mpango wa nyuklia , Marekani imeendelea kuhifadhi vichwa 20 vya makombora ya nyuklia na idadi kubwa ya wanajeshi kwenye ardhi ya Ujerumani tangu mwishoni mwa vita vikuu vya pili.