Vyama vinne vya upinzani vinavyounda Ukawa viko katika maandalizi ya Kuunda Chama kimoja cha siasa chenye nguvu zaidi.

Katibu wa Ukawa, Dk. George Kahangwa amesema kuwa kutokana na mafanikio waliyoyapata kupitia Muungano wao kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, vyama hivyo vimeanza kujiandaa kuwa chama kimoja cha siasa kinachotambulika kisheria.

“Sasa Ukawa inajiandaa kuwa chama kimoja cha siasa na tayari wanasheria wetu wameanza kuandaa maandiko ya kisheria yatakayopelekea kufanikiwa kwa mpango huo, alisema Dk. Kahangwa alipofanya mahojiano na gazeti la Mwananchi hivi karibuni.

Dk. Kahangwa ambaye ni mwanachama wa NCCR-Mageuzi, alisema kuwa Ukawa imefungua milango kwa vyama vingine vya vya upinzani kujiunga na umoja huo.

Ukawa unaundwa na NLD, NCCR-Mageuzi, CUF na Chadema. Umoja huo ukifanikisha kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani hadi kufikia 116.

 

Patoranking Anatafuta Mwanamke Wa Kuoa, Aelezea Sifa Zake
Profesa Jay Afunguliwa Kesi Mahakama Kuu