Harmonize ameupasua mtandao wa Instagram kwa mshangao baada ya kuweka wazi bei ya zawadi ya saa ya mkononi aliyonunuliwa na mpenzi wake, Sarah.
Kupitia kipande cha video alichoweka akiwa ughaibuni, mwanafamilia huyo wa WCB ameonesha saa aina ya Patek Philippe ambayo kwa mujibu wake imenunuliwa kwa $267,525 (sawa na shilingi milioni 603 za Tanzania).
Mwimbaji huyo ameweka picha ya inayoonesha saa hiyo yenye mng’ao wa ‘ukwasi’ na kuandika, “Put some respect on it, thanks baby @sarah__tz ❤ Google the price.”
Kwa lugha ya nyumbani Tanzania, Hamornize amemshukuru mpenzi wake Sarah kwa zawadi, ametaka anayeiona aipe heshima, lakini pia ametaka udhibitishe kwa kui-google.
Hata hivyo, alienda mbali na kusaidia kuiangalia kwenye Google ambapo ilionesha bei ya $267,525 huku nyingine ambayo ni tofauti na yake ikionesha bei ya $41,479.
Patek Philippe ni saa za adhimu na zenye gharama kubwa, awali bei ya saa zake ilikuwa kati ya $25,000 hadi $300,000.
- Aiba tuzo ya Oscar ya Muigizaji bora wa kike, polisi wapambana
- Marekani yaingilia kati mzozo wa kisiasa wa Ethiopia
Lakini hivi karibuni, iliibuka saa ambayo ilitikisha soko, gharama yake ikitajwa kuwa $2.5 Million, kwa mujibu wa Business Insider.
Ni Harmonize pekee na Sarah ndio wanaofahamu ukweli wa bei ya saa hiyo. Kama alivyowahi kusema Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, “akili ya mbayuwayu changanya na yako.”