Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi za Mifugo za Taifa, Prof. Philemoni Wambura kuvunja mikataba ya wawekezaji wa vitalu vyenye jumla ya hekta 68,238 kwenye ranchi ya Mkata na Dakawa ndani ya mwezi mmoja baada kushindwa kuviendeleza vitalu hivyo na kushindwa kuvilipia kodi kwa muda mrefu.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea katika ranchi ya Mkata na Dakawa kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika  katika ranchi hizo.

Amezitaja kampuni za wawekezaji  ambazo zilizomilikishwa vitalu zinatakiwa kuvunja mkataba kwa kushindwa kuendeleza upande wa ranchi ya Mkata katika Wilaya ya Kilosa kuwa ni pamoja na Kadolo Farm Company Ltd  kitalu namba 418 yenye hekta 4005, Bagamoyo Farm kitalu namba 419 yenye hekta 3672.96, A to Z Animal Feeds Company Ltd kitalu namba 420 yenye hekta 3692.97 na Ereto Livestock Keepers kitalu namba 422 yenye hekta 4020.54.

Aidha, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kumaliza  mara moja migogoro inayoendelea baina ya wakulima na wafugaji.

  • RC Makonda ajitolea kumpeleka Ahmed Albaity kutibiwa China
  • Magufuli afanya uteuzi mwingine
  • Video: Walisubiri mpaka nife ndio waje kuniona?- Lissu
  • Vile vile, amesema kuwa kama vyombo vya Serikali vingetumika vizuri kuanzia ngazi ya kijiji kungekuwepo na uwezekano wa kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika wilaya  hiyo.
  • Hata hivyo, amezitaka Halimashauri zote nchini kutotunga sheria kandamizi dhidi ya wafugaji, huku akitolea mfano wa sheria ndogo ya Halimashauri ya Mvomero ya kutoza faini ya shilingi 25, 000/=kwa kila mfugo kuingia  katika Wilaya hiyo bila kufuata taratibu.
  • Kwa upande wake, Katibu Mkuu Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Maghembe Makoye amesema upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya wafugaji utasaidia kuondoa migogoro baina ya pande hizo na kuendelezwa kwa ranchi za taifa.

Ni uzalilishaji mkubwa unaoendelea Libya- Nyalandu
Video: Ali kiba afanya kufuru, ni moja kati ya video kali 'Maumivu perday' haijawahi tokea