Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira. Luhaga Mpina amepiga marufuku shughuli za uchimbaji wa mchanga katika machimbo yaliyopo katika kijiji cha Kolangwa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kufuatia uharibifu wa mazingira na kuhatarisha maisha ya wananchi wanaozunguka machimbo hayo.

Mpina ametoa agizo hilo la kufungwa kwa machimbo hayo mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira mkoani Pwani ambapo amebaini uharibifu mkubwa wa mazingira uliosababishwa na machimbo hayo.

Aidha, ametoa wiki mbili kwa Taasisi za Serikali zinazohusika na utunzaji wa mazingira kukutana na mmiliki wa machimbo hayo kutathmini hasara aliyoisababisha ili aweze kulipa gharama za uharibu aliousababisha na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake ikiwemo kulipa fidia.

Hata hivyo, hapo awali Naibu Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha Azam kilichopo Mkuranga mkoani humo na kuupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa utunzaji wa Mazingira sambamba na hilo pia ameagiza kiwanda hicho kupima Maji taka yanayozalishwa kiwandani hapo.

 

Zitto: Bunge limezidi kusimangwa na serikali
Mrisho Mpoto atua China kwenye Tamasha la Utalii Duniani