Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amefuta tozo ya faini ya shilingi elfu hamsini kwa kila Ng’ombe mmoja na ameuagiza Uongozi wa Wilaya ya Singida kuwarudishia mara moja fedha wafugaji wote walizotozwa faini kinyume cha Sheria.
Mpina ametoa maagizo hayo hii leo mara baada ya kutembelea eneo la Hifadhi ya Msitu wa Jamii wa Mgori, kwenye Kijiji cha Handa na kuwaagiza Wakuu wa Mikoa ya Singida na Dodoma kupitia kwa Wakuu wa Wilaya ya Singida na Chemba kushughulikia tatizo la mipaka.
“Kama Waziri mwenye dhamana ya kushughulikia Sekta ya Mifugo na Uvuvi nchini sipo tayari kuvunja Sheria kwa kuwakumbatia wahalifu wanaokiuka Sheria za nchi, lakini pia wahalifu wanatakiwa kutozwa faini kulingana na Sheria na taratibu zilizowekwa,”amesema Mpina.
- Wizara ya Fedha na Mipango yashinda tuzo
-
JKCI kuwafanyia upasuaji wagonjwa wa moyo 80
-
LHRC champongeza JPM
Hata hivyo, ameongeza kuwa utozaji wa faini wa shilingi 50,000/= toka shilingi 20,000/= za awali kwa kila Ng’ombe aliyekamatwa na shilingi 25,000/= kwa Mbuzi toka shilingi 5,000/= za awali haukubaliki na kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Singida, Elias Tarimo kurudisha shilingi 30,000/= kwa kila Ng’ombe ambazo zimetozwa bila kufuata Sheria yoyote.