Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limepewa siku saba kukagua na kujiridhisha na uzalishaji na utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake kwa Kiwanda cha ANBANGS kinachotengeneza mifuko aina ya viroba vinavyotumika kama vifungashio vya saruji, sukari na aina nyingine ya nafaka, na kukifunga kwa kwa kukaidi maagizo ya Serikali ya awamu ya tano ya kutokulipa faini kwa uchafuzi wa mazingira.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa mazingira katika maeneo ya Sukita Mivinjeni Buguruni jijini Dar es salaam.
Aidha, Mpina amelitaka baraza hilo kupitia nyaraka zote muhimu zinazohusu kiwanda hicho ambacho awali hakikuwa na cheti ya tathmini ya athari ya mazingira wala vibali ya aina yoyote vya kutirirsha maji yaliyotibiwa na kuuganishwa na mfumo wa mji taka wa DAWASCO hali ambayo iliyopelekea wamiliki wa kiwanda hicho kufikishwa mahakamani.
-
Video: Mwakyembe amtumbua Malinzi wa BMT
-
Video: Majaliwa ategua kitendawili cha wakulima wa ufuta
-
Video: Mpina awapa miezi mitatu DAWASCO kurekebisha miundo mbinu yao
Hata hivyo, Katika Ziara za ukaguzi wa Mazingira na viwanda jijini Da es Salaam, Mpina ameahidi kushirikiana na mamlaka husika kuchukua sampuli za maji yanayopita katika bonde la mto msimbazi katika eneo la viwanda vya karibu na mtaa wa sukita mivinjeni ili kuyafanyia vipimo na kujirisha kama yana madhara kwa viumbe hai na mazingira hususani mboga mboga zinazomwagiliwa maji katika maeneo.