Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi Milioni thelalini na moja kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi la kupambana na uvuvi haramu.

Akizungumza mara baada ya kuteketeza nyavu hizo mapema, Mpina ameonyesha kushangazwa na suala la uvuvi haramu kuwa sugu kwani kama likivaliwa njuga linaweza kukomeshwa na kuokoa mazalia ya samaki wanaovuliwa kabla ya muda wao.

“kama nitashindwa kushughulia suala zima la uvuvi haramu, niitaaachia dhamana hii niliyopewa na Mheshimiwa Rais, na mpaka kufikia hatua hiyo lazima wengi watakuwa wamejuruhiwa.” Amesema Mpina.

Aidha, akiwa katika ziara ya operesheni maalum ya ondoa mifugo kutoka katika mikoa ya mipakani na nchi jirani akiwemo mkoani kigoma, Mpina  ametembelea mwalo mpya wa Kibirizi Mjini Kigoma na kumtaka Afisa Mifugo na Uvuvi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kushughulikia changamoto za mitambo wa kugandisha barafu inayokikabili kikundi shirikishi cha rasilimali za uvuvi mwaloni hapo.

 

 

Hata hivyo, zoezi la oparesheni ondoa mifugo na kukomesha rasmi uvuvi haramu limeanza rasmi kwa viongozi wa Wizara husika wakiongozwa na mawaziri Luhaga Mpina na Abdalah Ulega kuingia kazini katika mikoa inayokabiliwa na changamoto hizo.

Video: Itazame 'Mans Not Hot' ya Big Shaq
Waokolewa baada ya kukaa baharini kwa miezi mitano