Kiongozi Mkuu wa upinzni nchini Urusi, Alexei Navalny amezuiwa kuwania nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu mwakani,
Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa. Navalny hataweza kuwania kwa sababu alikutwa na makosa ya ufisadi ambayo anasema kuwa yamechochewa kisiasa,
Aidha, Mkuu wa tume ya uchaguzi, Ella Pamfilova amesema kuwa tume yake inatekeleza sheria ambayo inamzuia, Navalny kugombea nafasi ya kiti cha urais hapo mwakani.
Hata hivyo, Navalny amesema kuwa amekusanya sahihi 500 zilizohitajika kumwezesha yeye kugombea akiwa na matumaini kuwa hilo litaishinikiza tume ya uchaguzi kumruhusu kugombea.
-
Ajiua kwa kuhusishwa na kashfa ya rushwa
-
Mnangagwa amkomalia Rais Mugabe ajiuzulu
-
Mnangangwa: Huu si wakati wa kutambiana na kusifiana