Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amewataka Vijana kuwa na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara kwani kufanya hivyo kunapelekea Afya zao kuwa imara na kuepuka magonjwa yanayoweza sababisha vifo vya mapema.
Ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bonanza la Michezo maeneo ya Tabata lililoandaliwa na Windhoek beer, Mpogolo amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) vijana wengi wanapoteza maisha kwa kutotunza Afya zao na kueleza kuwa vifo takribani 3000 vimeripotiwa vinatokana na shinikizo la damu huku Tanzania ikiwa nchi ya 85,
Amesema kuwa ugonjwa wa kisukari una unagharimu maisha ya watu takribani 9257 wamepoteza maisha na Tanzania ikishika nafasi ya 35 kidunia na Kiharusi zaidi ya 5000 wanapoteza maisha na Tanzania ikishika nafasi ya 102 kidunia.
Kutokana na Takwimu hizo, Mpogolo amesisitiza mazoezi kwa vijana kwa kufanya michezo ambayo inawakutanisha na kuanzisha mahusiano ili kuleta undugu, huku akiwasisitiza waandaaji waandae mabonanza kama hayo yakishirikisha michezo ya aina mbalimbali siyo mpira wa miguu pekee.
Bonanza hilo lilikuwa kivutio baada ya Timu mbili za Kwetu Pazuri wakiwa wenyeji na Bongo Fleva, huku timu ya Kwetu Pazuri ikiwa na wachezaji ambao ni wasanii wa familia moja Ali Kiba na Abdul Kiba na mchekeshaji maarufu kama Kupe ambaye aliipatia ushindi Kwetu Pazuri kwa kushinda goli mbili kwa nunge, na kwa upande wa Bongo Fleva timu yao ilipambwa na mastaa wakongwe akiwemo KR, Mchizi Mox, Soggy Doggy, Suma G na Juma Nature.