Msanii wa muziki wa Bongo fleva Bizzy Babbylon Maarufu kama mr Blue anaetamba kwa sasa na bonge la track alilomshirikisha mkali wa bongo Ali kiba Kinng Kiba Mboga saba  amesema bifu hazina nafasi kwake hasa linapokuja swala la mtu ambaye ni zaidi ya rafiki kwake.

blue

Akizungumza katika mahojiano yake ya kipindi cha The Base cha ITV Mr Blue amesema Ali kiba ni zaidi ya Mwanamziki kwake, kwani yeye ndiye aliyempeleka studio kwa mara ya kwanza na maisha yake anamchukulia ni ndugu yake kwa sasa

”Ali kiba alikuwa akicheza mpira tuu mtaani, lakini aliwahi kuandika wimbo wa Abby Skillz wa maria nalia, na mwisho wa siku nlipojua baada ya Abby kuniambia nilimpeleka kwa enriko na baadae  tkaenda nae studio kwa G studio ambaye ndiyo iliyowatoa”.

Suala la bifu Blue amedai hujenga kama ni la kibiashara ni zuri kwani mtatengeneza attention na mwisho wa siku mkatumia kutengeneza pesa , ila kama ni la lachuki halina maana kwani mwisho wa siku linaweza kupelekea kifo.

Mr. Blue ni msanii aliyeanza muziki akiwa na umri wa miaka 15 mpaka sasa ana miaka 13 katika mziki wake na akiwa bado anazidi kufanya muziki mzuri kama vile Pesa, Baki na MImi, na mpaka sasa Mboga saba ambayo inazidi kumpa nafasi nzuri na kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa zamani waliobaki kwenye  ”game”

 

 

Kidole champonza Sugu, aadhibiwa kukosa vikao 10 vya Bunge, Kubenea naye nje
Wabunge wa Ukawa waja kivingine, ni nyeusi tupu na mabango