Shindano la kumtafuta MR. Tanzania linatarajia kufanyika Oktoba 22,2021 katika Ukumbi wa Kilimanjaro, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Shindano hilo Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mchezo huo toka (TBBF ), Francis Mapugilo, amesema kuwa shindano linatarajia kuanza saa moja asubuhi ambapo wadau mbalimbali wanatarajia kushiriki.

Mapugilo amesema kuwa kwa mwaka huu wameamua kufanya shindano hilo pekee kutokana na mdhamini kushindwa kumudu gharama za Mr. Tanzania, Mr. Physique pamoja na Miss Fitness.

Amesema kuwa kamati inaomba radhi washiriki ambao vipengele vyao vitakosekana kutokana na sababu zilizonje ya uwezo wao.

Katibu huyo amesema kuwa fomu za kushiriki zinapatikana katika kumbi za michezo mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Gym Bodyline Mikocheni, Gym Home Mwenge, Body Fuel Masaki pamoja na Gym zingine.

“Uhakika ni hivi bodybuilding safari hii itakuwa ni (Free Class) kwa maana hakutakuwa na groups kutokana na uzito wao “,amesema Mapugilo.
Amesema kuwa wamefanya hivyo kutokana na ufinyu wa bajeti ya mashindano , na kutakuwa na kipengele cha best Poser ilikuleta ladha kwenye shindano.

“Walio tayari kugombea wanatakiwa kulipa laki moja na hadi sasa maandalizi kupelekea siku hiyo yanaendelea vizuri,” amesema Mapugilo.
Amesema fomu zinapatikana kwenye wavuti yao www.tzbbf.org katika safu ya usajili pia unaweza kuipakua kwa bure.

Hata hivyo ameeleza kuwa mchezo kutunisha misuli ni miongoni ya michezo inayopendwa tangu mwaka 1990.

Mchezo huu ulitajwa kila kona, ndiyo ulioongoza kuwa na wadhamini wengi kuliko fani mengine ya burudani.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Pilipili Intertainment Millesh Batt, ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuja kuangalia shindalo la Mr. Tanzania.

Luis Miquissone: Sitaiacha Simba, ni familia yangu
Luniga kubwa kufungwa Chamazi