Meneja wa mradi wa kufua umeme wa Rusumo mhandisi Patrick Lwesya, ameeleza sababu ya kuwama kukamilika kwa wakati mradi huo kuwa ni kutokana na janga la Covid 19 ambapo mapema mwaka huu kufuatia janga hilo, wataalamu wanaojenga mitambo ya mradi huo waliondoka.

Lwesya ameeleza hayo wakati wa ziara ya mwenyekiti wa bodi ya shirika la umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika leo Septemba 14, kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi, ambapo amesema kuwa mradi huo unaendelea vizuri licha ya wataalamu wa masuala ya umeme kuondoka.

“Ujenzi wa mradi huu ulianza mapema kabisa kwenye masuala ya usanifu na kwa mujibu wa mkataba mradi huu ulitakiwa kukabidhiwa mwezi Februari mwaka huu, hali hiyo imeshindikana baada ya wataalamu wa masuala ya umeme na ufungaji wa mitambo hiyo kuondoka kutokana na ugonjwa wa Covid 19 ambao walikuwa wakitoka nchi za Ujerumani na India ambao wamekwama,” ameeleza Lwesya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Alexander Kyaruzi ameelezea kuwa mradi huo unarajiwa kukamilika Disemba 2021, na utazalisha mega wati 80 ambapo kila nchi mwanachama itachukua mega wati 27.

Mradi wa kufua umeme Rusumo unajengwa kwa mkopo wa dola za kimarekani 340 kutoka benki ya dunia, ambapo Tanzania italipa mkopo huo kwa asilimia 100%, Rwanda asilimia 50% huku Burundi ikiwa hailipi chochote na asilimia iliyobaki kutolewa kama ufadhili.

Wanafunzi ukunga kupewa somo
Jaji Mark Bomani azikwa, Majaliwa aongoza waombolezaji