Mradi wa majaribio wa miezi 15 wa watoto ambao hawakupata nafasi ya kwenda shule umezinduliwa mkoani Tanga, kwaajili ya kuwawezesha kujifunza wenyewe kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotumia tableti.
Uzinduzi wa Mradi huo umefanyika katika kijiji cha Zenith ya Kati, Wilayani Muheza, ambapo ni sehemu ya mradi mkubwa wa miaka mitano wa majaribio duniani chini ya Global Learning Xprize wenye lengo la kutatua matatizo ya kujifunza.
Mradi huo hapa nchini unaendeshwa kwa pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na XPrize.
Aidha kuwezekana kuwapo kwa mradi huo kumetokana pia na makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na mashirika hayo.
-
Mpina afuta tozo za mifugo zisizozingatia sheria
-
Waaswa kulinda rasilimali za taifa
-
LIVE: Miili ya wanajeshi 14 waliouawa DRC ikiwasili Tanzania
Hata hivyo, Katika utoaji wa elimu hiyo watoto wanaohusika ni wa miaka kuanzia 9 hadi 11 na watajifunza kwa kutumia program tano zilizowekwa katika tableti zitakazomuwezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu