Serikali imemtaka mrajisi wa Vyama Vikuu vya Ushirika kufikia Mei 30 awe amemaliza migogoro yote iliyoko na wawekezaji ambao wamekuwa chanzo cha migogoro katika vyama hivyo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe leo Mei 2,2023 bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Hai Sashisha Mafuwe aliyehoji Ni lini Serikali itamaliza migogoro kwenye vyama vya Ushirika Makoa, Ndososangi, Mkundoo ili wakulima waendeleea na kazi yao ya kulima?
“Serikali inaendelea kuchukua hatua za kisheria ili tuweze kuwachukulia hatua za kisheria kwa sababu wao kuwa wawekezaji hatuwezi kuwaruhusu waweze kutumia nafasi hiyo kuweza kuathiri vyama vya ushirika na kuruhusu ubadhirifu unaondelea katika vyama hivi”
Aidha Waziri Bashe amesema kuwa mrajisi wa vyama vikuu vya ushirika anafahamu na amepewa muda wa kutatua migogoro hiyo.
”Asipochukua hatua chukua hatua za kinidhamu kwa viongozi wa vyama hivi serikali itamchukulia hatua yeye na tutamshauri Mhe. Rais amuondoe katika nafasi hii kwa sababu nafasi aliyonayo ni ya uteuzi wa Rais”.
”Ni kweli kwamba kwenye chama cha ushirika cha Kikafu chini, Mrososangi, Mkuu, Chama cha Makoa na baadhi ya vyama vingine katika mkoa wa Kilimanjaro, kuna migogoro ambayo inaendelea na serikali imemtaka mrajisi wa vyama vya ushirika kumaliza migogoro iliyopo ifikapo mei 30”.