Mratibu mkuu wa vikwazo nchini Marekani dhidi ya Iran, Sigal Mandelker anayefanya kazi katika Wizara ya Fedha ameripoti kujiuzulu nafasi yake hivi karibuni.

Gazeti la Kimarakeni la Wall Street Journal limeripoti habari hiyo ya kujiuzulu  kwake ndani ya wiki kadhaa zijazo na hivyo kuhitimisha kuitumikia serikali ya Rais Donald Trump.

Pia gazeti hilo limemtaja mwanamke huyo kuwa mwenye nafasi kubwa katika kutekeleza vikwazo vya kifedha dhidi ya Iran.

Sigal Mandelker alianza kufanya kazi katika ofisi ya kupambana na ugaidi na taarifa za kifedha ya Marekani pamoja na ofisi ya Vita vya Kiuchumi vya Washington dhidi ya Iran hapo mwaka 2017 kwa kumuunga mkono Trump, mbali na hayo Mandelker alibeba jukumu la mratibu mkuu ndani ya wizara hiyo.

Aidha, itakumbukwa kuwa serikali ya Marekani ilichukua hatua ya upande mmoja ya kujiondoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia JCPOA tarehe 8 Mei mwaka jana, kinyume kabisa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kisha kuiwekea vikwazo vikali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hii ni katika hali ambayo hadi sasa serikali ya Marekani imeshindwa kufikia malengo yake dhidi ya Iran katika vikwazo vyake hivyo.

Korea Kaskazini yafyatua kombora zito, linaweza kubeba nyuklia
Trump awawakia wabunge, adai kuna mtu anampeleleza Ikulu