Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TPL), Augustine Mrema amekiri kuwa nguvu ya umma inayoonekana kumsapoti mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa ni zaidi ya ile iliyomsapoti wakati wa uchaguzi Mkuu mwaka 1995.

Mrema alikuwa huo alikuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha NCCR – Mageuzi ambapo alionekana kuungwa mkono na maelfu ya watanzania dhidi ya mgombea wa CCM, Benjamini Mkapa. Vijana wengi walijitokeza kumuunga mkono huku wengine wakisukuma gari lake kilometa kadhaa likiwa limezimwa.

Mrema amejitokeza na kupingana na kauli za viongozi wa CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyedai kuwa umati unaoonekana kumsapoti Lowassa hivi sasa hauikitikisi chama hicho kwa kuwa ni kama ule uliojitokeza kumsapoti Mrema mwaka 1995 lakini akashindwa katika uchaguzi huo.

Mrema alieleza kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya wakati ule na wakati huu na kwamba hivi sasa vijana wengi wanaoonekana kumsapoti Lowassa wamejiandikisha na watapiga kura.

“Wakati ule walikuwa na Bba wa Taifa aliyewasaidia, safari hii sijui wako na nani wa kuwapa ushindi. Maana tayari wamesema watatumia bao la mkono na hata Bwana Mkubwa (Rais Kikwete) ameshasema kasi ya wapinzani ni moto wa mabua, pengine wameshapata dawa ya kuuzima huo moto wa mabua,” alisema Mrema.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa TLP alidai kuwa alishinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 lakini aliibiwa kura na kufanyiwa hujuma kwa kuwa hakuwa na uzoefu wa kujua mbinu za ushindi zilizonywa na CCM.

Koeman: Kumuuza Mane Ni Sawa Na Uwendawazimu
Azam FC: Suala La Muamuzi Sio Kazi Yetu