Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema, ameibuka na kusema kuwa wapo baadhi ya polisi wanagawa na kusambaza dawa za kulevya pia wanawasaidia baadhi ya waathirika wa dawa hizo waliopo magerezani kuzipata.
Mrema amesema vita ya dawa za kulevya inawezekana kumalizika kama watawatumia watumiaji na wauzaji wadogo wadogo kuwapata wale wauzaji wakubwa ambao ndiyo tatizo zaidi katika jamii.
“Vita hivi vitawezekana kumalizika kama tutatumia hawa wadogo wenye kete mbili mbili, na siyo kuwapeleka magerezani, wamenionesha na njia wanazotumia kuwapa dawa waathirika waliopo magerezani, tusitumie nguvu nyingi kuwakamata hawa dagaa wadogo wadogo, bali tuwatumie hawa tupate mfumo mzima, kwa njia hiyo tutapeleka watu wanaostahili magerezani” amesema Mrema.
Aidha, Mrema amesema kama polisi walikuwa wanasambaza na kugawa madawa ya kulevya hivyo basi wao ndiyo walikuwa wakiendesha hivyo vijiwe na wanawajua wahusika wa madawa ya kulevya.

Mpango: Hali ya uchumi ni mbaya kusini mwa jangwa la sahara
Avram Grant Aachana Na Black Stars