Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amepewa mchongo namna ya kumtumia staa wake mpya, Kai Havertz ili afanye vizuri msimu ujao 2023/24.

Arsenal ilinasa saini ya Havertz kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi akitokea Chelsea kwa ada ya Pauni 65 milioni na kinachoonekana ni kwamba miamba hiyo ya Emirates bado haijapata mahali panapomfaa kucheza Mjerumani huyo na kuonyesha ubora mkubwa ndani ya uwanja.

Lakini, mtangazaji wa televisheni TNT Sports, mrembo, Laura Woods amemwambia Arteta wazo lake la kumchezesha Havertz kwenye kiungo si mbaya, lakini asifikirie kabisa kumtumia kwenye nafasi ya ushambuliaji.

Havertz alitumika kwenye nafasi ya ushambuliaji kwenye kikosi cha Chelsea msimu kwa mzima na hakuonyesha ubora wa kutosha wa kufunga, hivyo si eneo ambalo litaonyesha ubora wake halisi ndani ya uwanja.

Wakati anamchukua kwenda Arsenal, Arteta alisema Hazertz atakwenda kutumika kwenye kiungo, nafasi ambayo aliwahi kucheza huko nyuma kitu ambacho kinaungwa mkono na mrembo Laura, akisema: “Nadhani Havertz sio straika, nadhani anaweza kucheza wingi ya kulia. Kama Arteta anadhani anaweza kucheza kiungo, basi nitamwamini Arteta. Siku zote nimekuwa nikiamini katika mipango yake.”

Hilo limekuja baada ya Havertz kuwa gumzo kwa siku za karibuni baada ya uhamisho wake wa kutoka Chelsea kutua Arsenal.

Lakini, mrembo Laura amesema kinachokwenda kutokea kwa Havertz ni kama kile cha Joelinton aliponaswa na Newcastle United kama Mshambuliaji, lakini baadae akaanza kutumika kwenye kiungo.

George Mpole ajiandaa kukiwasha DR Congo
Matumizi bidhaa za Chuma yaongezeka