Mwanamuziki na mwigizaji nyota wa Afrika Kusini Nadia Nakai ameshiriki kumbukumbu ya kihisia kuhusu mpenzi wake marehemu Kiernan Forbes maarufu AKA ambaye alifariki kwa kupigwa risasi takribani wiki moja na nusu iliyopita huko Durban Afrika Kusini.

Nakai na AKA walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda kabla ya kifo cha rapa huyo na wawili hao hawakuwahi kukwepa kudhihirisha ukaribu wao kwa kushiriki video na picha mbali mbali wakiwa katika kujiburudisha pamoja.

AKA alizikwa Februari 18, 2023, mchumba wa marehemu rapa huyo amelazimika kuutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kwa mara ya kwanza kuweka wazi hisia zake hadharani kuhusu AKA punde baada ya mazishi yake.

“Moyo wangu umevunjika, hii sio jinsi maisha yetu ya baadaye yalivyokusudiwa kuonekana. Siwezi kuamini kuwa nilikuaga kwa mara ya mwisho.

Sitakuona tena kwenye maisha yangu yote? Ulinipenda kwa sauti na kiburi, asante. ulinilnda, ukaniombea, ukanitia moyo,” aliandika Nadia.

AKA alikuwa akijitokeza wakati wa maonyesho ya Nakai na alikuwa akimchangamsha kila mara alipokuwa karibu.

Pichani ni mrembo Nadia Nakai akiwa na rapa AKA enzi za uhai wake

“Naona ugumu hata kupumua ninapotafuta maneno ya kuelezea jinsi ninavyokupenda. Kwa kweli nitakukosa katika nyakati zote maalum ambazo tumewahi kuwanazo. Hii inaumiza sana!

“Siwezi kukubaliana na ukweli kwamba sitawahi kusikia ukisema unanipenda, sitawahi kisikia tena kicheko chako, Tulikuwa na mipango,” aliongeza Nadia.

Nadia alihitimisha kwa kuweka wazi kuwa alitarajia kuwa angetumia maisha yake yote akiwa na AKA japo imekuwa kinyume na hali halisi.

Mashabiki wa nyota hao kwa kiasi kikubwa wameonyesha kuamini kwamba Mungu aliwatumia wawili hao kuuonyesha ulimwengu jinsi mapenzi ya kweli yasiyo na masharti yalivyokuwa, licha ya Nadia kumhoji Mungu katika heshima yake kwa AKA.

“Hakuna maumivu makubwa zaidi ya kukupoteza. Nilidhani nitaenda kukaa na wewe maisha yangu yote, natambua wewe ndiye uliyekuwa na mimi maisha yako yote, sijui. kwa nini mambo yanatokea jinsi yanavyotokea, lakini ninamhoji Mungu sasa hivi.

“Kwanini atukusanye ili akuondoe tu sielewi, sijui nitafanyaje naendelea na maisha yangu bila wewe siwezi, Kiernan, nakupenda,” alihitimisha Nadia.

Rapa AKA ameacha mtoto mmoja, Kairo Owethu Forbes ingawa tetesi zinasema kuwa Nadia ni mjamzito.

Eric Omondi atiwa mbaroni, sakata la kuzua ghasia Kenya

Trump adai atamaliza vita vya Ukraine kwa siku moja
Uwanja wa Benjamin Mkapa upo hatarini