Msichana mmoja anaedaiwa kuwa mrembo wa sura na raia wa Uingereza, amekiri mbele ya mahakama jijini Manchester kuwa yeye ni gaidi na anamiliki vilipuzi.

Ripoti kutoka jijini humo zinaeleza kuwa msichana huyo aliyekuwa anakabiriwa na mashtaka mawili, moja la kumiliki nakala ya kitabu cha ‘Anarchist CookBook’ chenye maelekezo ya kutengeneza bomu na kumiliki vilipuzi pamoja na kupanga njama ya kufanya ugaidi, alikiri mashtaka yote.

Mapema Aprili mwaka huu, kitengo cha kukabiliana na ugaidi cha kaskazini magharibi mwa Uingereza kilimkamata msichana huyo pamoja na mvulana wa miaka 14 ambaye pia alikiri kuhusika katika njama ya kuwashambulia polisi katika gwaride nchini Australia.

Dibaba Atwaa Medali Ya Dunia mita 1500
Rais Wa FC Barcelona Awawekea Ngumu Man Utd