Picha zinazomuonesha mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam akiwa katika hali ya kutisha zimetumiwa kufanya upotoshaji kwa kumzushia msichana mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Picha iliyounganishwa ikionesha taswira ya msichana huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakidai kuwa hapo ni kabla zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasio na nia njema na kusababisha usumbufu kwa mrembo huyo.

Msichana huyo ambaye anatumia jina la Ms.Adelaide kwenye Instagram amekanusha vikali taarifa hizo huku akieleza kwa uchungu jinsi ambavyo ameathiriwa na uzushi huo.

NAJUA WENGI MTAKUA MMEKUTANA NA HIZI HABARI..SIJAJUA NANI ALIEANZISHA HII MADA NA SIJUI IMEANZIA KWA NANI. MIMI NI MZIMA NA SIO MSUKULE JAMANI? NINA WAZAZI WOTE WAWILI WAPO HAI NA WAMEUMIZWA SANA NA HIKI KITENDO, MY FAMILY MEMBERS WAMEUMIA MNOOO KUPITA KIASI, LICHA YA HIYO MIMI BADO NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU, WANAFUNZI WENZANGU WENYE MAPENZI NA MIMI WANAUMIA SANA PIA WANAPOONA MAMBO KAMA HAYA. PLEASE ACHENI KUENDELEZA HIZI HABARI ZA UONGO, TUSIPELEKANE MPAKA TCRA SASA MAANA TUTAKUA TUNAPOTEZEANA MUDA,” aliandika Instagram na kuambatanisha na picha hii;

 

Mrembo-Msukule

Membe adai Magufuli anawafukuza watumishi kirahisi kwakuwa hakuwateua yeye
Membe aunga jambo 'kilio' cha Lowassa