Ushabiki wa timu hasimu za wasanii wa Bongo Flava nchini kumemuogofya mkali wa kughani na kutunga mashairi, Mrisho Mpoto ambaye ni mmoja kati ya waliotajwa kuwania tuzo za AFRIMMA (African Muzik Magazine Awards).

Mpoto ameweka wazi hisia zake kwenye Instagram alipokuwa akiwafikishia mashabiki wake habari njema za kutajwa kuwania tuzo za AFRIMMA katika kipengele cha ‘Best Traditional Artist’.

“Kungwi yeye kafundishwa na nani mbona anafundisha wengine?” Nimetajwa kwenye tuzo za Afrimma, sijui kama ntafurukuta maana nchi yetu imeshakua nchi ya mateam now days!! eeeh mungu nisaisaidie! ! #afrimma.”

Huenda hofu ya Mpoto ikawa na maana kubwa endapo timu maarufu mitandaoni (Timu Ali Kiba na Timu Diamond) zitajikita katika ushabiki wa wasanii hao wawili pekee katika kupiga kura na kuhamasisha watu kwa ushabiki na kusahau vipengele vingine wanavyoshindania wasanii wa Tanzania.
Diamond na Ali Kiba wanachuana katika tuzo hizo kubwa zitakazotolewa Marekani, katika kipengele cha ‘Best Male East Africa’ huku Diamond akiongozwa kwa kutajwa zaidi.
Wasanii wengine wa Afrika Mashariki walio kwenye kipengele hicho ni Eddy Kenzo (Uganda), Jaguar (Kenya), Bebe Cool (Uganda), Jackie Gosse (Ethiopia), Ali Kiba (Tanzania) Dynamq (South Sudan).

Juventus Wafunguliwa Dirisha Kumalizana Na Julian Draxler
AS Roma Yamnyemelea Wojciech Szczesny