Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC tayari wamepata kocha mpya ambaye atarithi mikoba ya aliyekuwa kocha wao, George Lwandamina.

Ambaye ni Zahera Mwinyi kutoka DRC mwenye uraia wa Ufaransa, na tayari amekwishatua jijini Dar es salaam kujiunga na timu hiyo tangu jana Aprili 24, 2018.

Kabla ya kujiunga na Yanga SC, Zahera alikuwa ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya DRC pia amewahi kufundisha DC Motema pembe ya nchini humo.

Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten amesema kocha huyo bado anaendelea na mazungumzo na katibu Mkuu wao Boniface Mkwasa na baada ya hapo kila kitu kitawekwa hadharani ikiwa ni pamoja na muda wa mkataba atakaopewa.

Kocha huyo mtihani wake wa kwanza utakuwa ni kutetea taji la ligi kuu Tanzania (VPL) kwa kuanza na mcheezo dhidi ya watani zao wa jadi, Simba utakaopigwa Aprili 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Zahera amesema mechi dhidi ya Simba haimtishi kwani ana uzoefu wa kupambana katika mechi ngumu za aina hiyo, hivyo kwa upande wake hakutakuwa na jipya.

 

Chadema wadai hawahusiki na maandamano
Ujumbe mzito aliotumiwa bilionea Msuya kabla ya kifo chake