Gari la Waandishi wa Habari waliokuwa kwenye msafara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, imepata ajali maeneo ya Mtule walipokuwa wakielekea Mkoa wa Kusini.

Kufuatia ajali hiyo, Fundi Mitambo kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Khamis Machenga amefariki Dunia na Watu wengine takribani watano wamejeruhiwa.

Majeruhi wamekimbizwa Hospitali ya Mnazi mmoja na tayari Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman, amefika Hospitalini kuwajulia hali.

Aidha, waliojeruhiwa ni mpigapicha Kassim na mwandishi wa habari Hassan Issa, wote kutoka ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Ajali hiyo imetokea eneo la Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja.


Masharti magumu kambini Young Africans
Nchimbi aondolewa Taifa Stars