Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan uliokuwa ukitoka Ikulu ndogo ya Rais Mkoani Mtwara kuelekea wilaya ya Tandahimba umepata ajali na kusababisha majeruhi.

ajali2

Majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Nanguruwe wilaya ya Mtwara walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Ligala.

Imeelezwa kuwa gari lilikuwa limewabeba wasaidizi wa Makamu wa Rais liliacha njia na kupinduka muda mfupi baada ya gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari kunusurika kupinduka.

Chanzo cha gari hilo kupinduka bado hakijaelezwa kiundani lakini inatajwa kuwa huenda ubora duni wa barabara ulichangia kutokea kwa ajali hiyo.

 

 

Kocha Mohammed Msomali Azikwa
Ummy Mwalimu Alitaka Baraza La Famasia Nchini Kuwafutia Usajili Wafamasia Wanaokiuka Kanuni na Taratibu za Baraza Hilo