Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam SACP Lazaro Mambosasa, amekanusha taarifa zinazodai kutekwa kwa msaidizi wa Bernard Membe, Jerome Luanda na amesema kuwa yuko mikononi mwa polisi na ni mzima wa afya.

Mambosasa amesema kuwa msaidizi huyo yuko mikononi mwa polisi kwa kosa la utakatishaji fedha na alikamatwa katika uwanja wa Ndege Julius Nyerere.

“Huo ni uongo, uzushi, tumemkamata akiwa Airport pale Julius Nyerere nasikia wengine wanasema wamemtafuta vituo vyote hawajamuona ni uongo, sisi tupo naye na ni mzima wa afya, tunamshikilia kutokana na kesi zake ambazo hatuwezi kuzitaja,” amesema Mambosasa.

Hayo yanajiri baada ya mgombea Urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo Bernad Membe, kuandika katika ukurasa wake wa Twitter mnamo Septemba 16, 2020 kuwa msaidizi wake amechukuliwa na watu wasiojulikana, na kutoa masaa kadhaa ili kupatikana kwa msaidizi wake huyo.

Young Africans yawasili Bukoba
Afrika Kusini kufungua mipaka yake Oktoba 1