Baada ya kukamilika kwa siku ya tatu ya msako wa ndege iliyopotea ikiwa na mchezaji Emiliano Sala wa Klabu ya Cardiff City, kikosi cha uokoaji kimehitimisha rasmi zoezi hilo.

Polisi wameeleza kuwa baada ya kukamilisha saa 80 za msako mkali, hawana budi kutia nanga kwani juhudi zao zimegonga mwamba.

Ndege binafsi iliyokuwa imembeba mchezaji huyo kutoka Nantes ilipotea Jumatatu, baada ya kupoteza mawasiliano ikiwa angani katika umbali wa maili 8 kaskazini mashariki mwa kisiwa cha Guernsey.

Mapema leo, msemaji wa kisiwa cha Burhou alisema kuwa msako mkali uliendelea kwa ndege na kwa miguu katika kila eneo walilolifikiria, lakini alikiri kuwa matumaini ya kumpata mchezaji huyo au rubani wa ndege hiyo, Dave Ibbotson.

Msemaji huyo anayefahamika kwa jina la David Barker alisema kuwa muda wa wawili hao kuweza kuishi ndani ya maji ulikuwa unakaribia kuisha, hivyo kuwapata wakiwa hai inaweza kuwa vigumu.

“Kama kikosi cha utafutaji tunasema, muda wa kuishi ndani ya maji ya bahari ni mdogo, tunakadiria kuwa baada ya saa uwezekano wa kuendelea kupigania maisha ndani ya maji utakuwa mgumu,” alisema David.

Sala alikuwa anasafiri kutoka Welsh/Wales baada ya kusaini mkataba wa kuichezea Cardiff City kwa £15 milioni, akitokea Nantes lakini ndege aliyokuwa akiitumia ilipoteza mawasiliano na hadi sasa haijapatikana.

Angalia hapa matokeo kidato cha nne, seminari yafutiwa
Rais mpya wa DRC augua ghafla baada ya kuapishwa

Comments

comments