Maafisa usalama wa Baltimore huko jimbo la Maryland nchini Marekani, wanaendelea kuwatafuta washukiwa wa shambulizi lililotokea mapema Jumapili, wakati wa sherehe zilizofanyika katika mtaa mmoja mjini humo.

Kaimu Mkuu wa Polisi wa Baltimore, Richard Worley amesema watu 20 miongoni mwa waliojeruhiwa na waliweza kutembea wenyewe hadi hospitalini.

Amesema, “watu wawili waliuawa na wengine 28 kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi wakati wa sherehe kwenye mtaa wa kusini mwa mji huo, wa Brooklyn Homes.

Meya wa Baltimore, Brandon Scott amewaambia Waandishi wa Habari kuwa tukio hilo linaangazia umuhimu wa kushughulikia tatizo la umiliki wa bunduki, wa eneo hilo na kote nchini humo.

Dodoma Jiji: Tutakuja kivingine 2023/24
Prince Dube bado yupo sana Azam FC