Mwanasheria na Wakili wa kujitegemea, Albert Msando amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa miongoni mwa watu 9 ambao watakuwa na jukumu la kufuatilia na kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kote nchini.
 
Msando ameandika ujumbe huo wa shukrani kwenye ukurasa wake wa instagram, na kusema kuwa anaamini kazi hiyo itafanyika kwa weledi.
 
“Namshukuru Dkt. John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uteuzi wa kuwa mjumbe wa Tume ya Kufuatilia Mali za Chama. Chini ya Mwenyekiti Dkt. Bashiru Ally Kakurwa na wajumbe wengine wa tume, nnaamini kwa dhati kazi hii itafanyika kwa weledi ili kukiwezesha chama cha Mapinduzi kujitegemea kupitia mali zake,”ameandika Msando
 
Rais Magufuli ameteuwa timu ya watu 9 ambao wataunda tume ya kufuatilia na kuhakiki mali za CCM nchini kote, baada ya kubaini kuna baadhi ya mali haziingizi kipato stahiki.

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 22, 2017
Tanzania yazidi kuporomoka viwango vya soka