Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amemchagua Mwanasheria na mdau wa masuala ya Sanaa Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya hakimiliki.

Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara Bi Leah Kihimbi kuhusu uteuzi huo wa Msando imesema kwamba uteuzi huo umetokana na vikao vilivyofanywa na wadau wa sanaa pamoja Mh. Waziri Mwakyembe.

Kupitia ukurasa wake wa Istagram Alberto Msando amesema kwamba ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria za nchi zinalinda haki za wasanii na kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao.

“Ulaya na Marekani wasanii wengi sio masikini. Hapa kwetu wasanii wengi ni majina tu. Wengi wanaishi maisha ya naomba nitoe niko vibaya, ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria zetu zinalinda haki za wasanii,” ameandika Msando katika ukurasa wake wa Instagram.

Mara nyingi Msando amekuwa mbele katika kuwasaidia wasanii kwenye masuala yanayohitaji msaada wa kisheria.

Video: JPM afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu
Wawili wajeruhiwa baada ya Ndege waliyopanda kuanguka