Nyota wa muziki wa bongo fleva na mmiliki wa lebo ya Wasafi, Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Planumz amesisitiza kuwa taratibu zinaendele kuzingatiwa kwa msanii yeyote anayesimamiwa na rekodi lebo hiyo na kisha kuamua kuondoka.

Katika mahojiano aliyofanya na kituo cha Wasafi Tv Diamond amesema kuwa mwanzoni uelewa wa sehemu kubwa ya wadau na mashabiki kuhusu biashara ya muziki ulikuwa chini na ndio sababu alipitia kipindi cha kulalamikiwa kuwa anawanyonya wasanii waamuapo kujitoa katika lebo hiyo ya WCB.

“Pengine mwanzo ilikuwa ni upya wa Industry watu kutoelewa, nakumbuka wakati mmoja msanii mmoja wakati anatoka, akawaambia kwamba anatakiwa kulipa kiasi cha pesa, sasa wale walikuwa hawajujua vizuri nikakutana nao nikawaambia kuna miziki miwili, kuna muziki na muziki ndani ya Wasafi, Muziki ndani ya wasafi watu wanapata riziki”

Nikawaambia huyu msanii unayemzungumza sasa hivi YouTube yake kwa mwezi inatengeneza sio chini ya milioni arobaini na nane, wewe unaniambiaje kila mwezi hiyo Milioni arobaini na nane niiache, msanii hawezi akaondoka hivi hivi, nimewekeza hela yangu ya kutosha mpaka anafanikiwa na kuingiza Mamilioni Ya Fedha” Amesema Platnumz

Hadi sasa jumla ya wasanii watatu walijitoa ndani ya WCB na kuamua kujisimamia wenyewe kundesha shughuli zao za muziki

Mwimbaji huyo mwisho mwa juma lililopita alifanya hafla ya kumtambulisha rasmi msanii wake mpya D voice, hafla iliyoudhuriwa na wasanii na watu mashuhuri kutoka katika tasnia mbali mbali.

Watch: Diamond lane London kwenye exclusive interview na ThePlug ya Dar24Media

Wanafunzi wanusurika kifo Muleba, Bweni lateketea
Holcim Group yaiweka sokoni Mbeya Cement