Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Omo Alhaji,Jagabana maarufu YCEE,ametoa msaada wa shilling million 1,kwa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Kigamboni Community Center(KCC).

Akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo leo jijini Dar es salaam mratibu wa ujio wa msanii huyo bi Salha Kibwana amesema kuwa msanii YCEE ametoa msaaada huo katika kituo hicho kwa lengo la kusaidia watoto hao ili kujipatia mahitaji maalum ya kila siku wawapo kituoni hapo.

“Ametoa msaada huo kutokana na faaida anayopata katika kazi zake usanii ili kukuza vipaji na kujenga upatikanaji wa elimu wa elimu kwa jamii hasa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi,”alisema Salha

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa kituo hicho Mbwana Msangule,amesema kuwa kituo chake kinalea watoto hao ili kuwasaidia kuondokana na maisha magumu yanayowakabili.

“msaada huu utasaidia sana kwasababu kituo kina watoto 14 wanaoishi kituoni hapo na wengine wanakuja na kurudi makwao,na nashukuru sana kwa msaada huu kwani ni sanii wa kwanza  kutoka msaada,nawaomba pia wasanii wa ndani kijitokeza kutoa msaada”alisema Mbwana

Kwa upande msanii huyo amesema kuwa amekuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuonana na wasanii wengine wakubwa wa Tanzania huku akiwataja Diamond na Ali Kiba,ameongeza kuwa amefurahi pia kuktana na mashabiki wake ambao amekua wakichati kupitia mitanzandao ya kijamii.

Nape Awataka Watanzania Kuwa Wazalendo
Vyombo Vya Sheria Vyatakiwa Kuwasaidia Watumiaji Madawa Ya Kulevya