Kama wewe ni msanii wa Tanzania na unataka kuendelea kimuziki katika ulimwengu wa kimataifa, kupata collabo na wasanii wakali kutoka Nigeria pamoja na video zako kuchezwa katika kituo cha kimataifa cha MTV, hupaswi kuanzisha bifu ya wazi na Diamond Platinumz.

Hayo yamebainika baada ya msanii huyo kuweka wazi kuwa vituo vingi vya kimataifa humtumia yeye kuidhinisha wimbo upi wa Tanzania uchezwe katika runinga hiyo na ipi isichezwe.

“Nikiamua kubana mbona naweza tu. Kwa sababu vituo vingi vya nje vinanisikiliza mimi. Kwa mfano MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yeyote kutoka hapa Tanzania wananipigia wananiuliza huyu vipi,” tuicheze ngoma yake au la? Mimi huwa nasema tu anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza. Nikiamua kubana si nabana tu?”, Diamond anakaririwa.

Diamond aliongeza kuwa kila collabo inayofanywa na msanii wa Tanzania na wasanii wa Nigeria yeye ndiye anayewezesha.

Baba Tiffah alitoa maelezo hayo wakati akikanusha kuwa huwabania baadhi ya wasanii ili wasifanye vizuri kimataifa kama yeye.

Hii inaonesha dhahiri kuwa endapo Diamond ataamua kumuwekea msanii bifu kweli, basi msanii huyo atapiga mark time kando ya mipaka ya Tanzania.

Ligi Ya England Inaendelea Kustaajabisha
Msanii huyu wa Bongo Movie aamua kumpa Figo mama yake