Mwimbaji maarufu, muafrika aishie jijini New York nchini Marekani jana alitangazwa kuwa moja kati ya washindi wa tuzo za Grammy 2016 akiibeba tuzo hiyo kwa mara ya tatu.

Angelique Kidjo, ambaye ni raia wa Benin anayefundisha muziki nchini Marekani, ameshinda tuzo ya ‘Best World Music Album’, kupitia album yake ya ‘Sings’ yenye mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali zilizotayarishwa kwa mchanganyiko wa mtindo za kiutamaduni/asili.

Mwimbaji huyo aliyeitoa Afrika Kimasomaso kwenye tuzo hizo, alipanda jukwaani… hakupewa tuzo nyuma ya jukwaa kama ilivyozoeleka kwa BET, na kuzungumza mawili matatu baada ya kucheza wimbo wa Jams Brown, ‘I Feel Good’.

“Napenda kui-dedicate tuzo hii ya Grammy kwa waimbaji wote wa nyimbo za asili barani Afrika, nchini kwangu na kwa kizazi kipya,” Kidjo alisema. “Afrika imepaa, Afrika iko Chanya, Afrika ni yenye furaha,” aliongeza.

Katiba Mpya; NEC yatangaza kuanza mchakato wa kura ya maoni
Tanzia: Msanii Joni Woka afariki