Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI, imeitaka Bohari Kuu ya Dawa Nchini – MSD, kuongeza kasi ya usambazaji wa bidhaa za Dawa pamoja na kuwa na maghala ya hitaji hilo kwa kila Halmashauri.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI, Stanslaus Nyongo ametoa rai hiyo baada ya kupokea taarifa ya usambazaji wa bidhaa za Afya kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai katika kikao cha Kamati kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.

Amesema, “naipongeza sana Wizara kwa hatua mnazoendelea kuchukua za kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za Dawa na vifaa tiba inaongezeka lakini pia niwatake muongeze jitihada hizo kwakuwa uhitaji wa bidhaa hizo ni mkubwa nchini.”

Akijibu maswali ya Wajumbe wa Kamati hiyo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali imeipa mtaji MSD ili kuhakikisha Dawa na vifaa tiba zinapatikana kwa wakati na kusambazwa nchini na kwamba amepokea mapendekezo yote na yatafanyiwa kazi.

Akiwasilisha taarifa kwa kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa – MSD, Mavere Tukai  amesema usambazaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupitia Mfumo wa Ugavi Shirikishi umefanikiwa kwa asilimia 97.

MAISHA: Bwawa la kuogelea Pombe kuponya jeraha
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 16, 2023