Mifumo ya upatikanaji na usambazaji wa bidhaa za Afya umeimarika hadi kufikia asilimia 64 2023 ikilinganishwa na asilimia 51 ya mwaka 2022. ambapo upatikanaji wa Dawa umepanda hadi kufikia asilimia 81 kwa mwaka 2023, ikilinganishwa na asilimia 57 ya Juni, 2022.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),Mavere Tukai alipokuwa akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam leo Septemba 27, 2023 nakuongeza kuwa Vilevile ongezeko la fedha kwa ununuzi wa bidhaa za afya, fedha iliyopokelewa mwaka wa fedha 2022/23 ni Sh. bilioni 190.3 ikilinganishwa na Sh.Bilioni 134.9 mwaka wa fedha 2021/22 sawa na asilimia 95.
Amesema, “utekelezaji wa mradi wa Ununuzi na Usambazaji wa vifaa vya huduma kwa wajawazito wanaopata uzazi pingamizi wakati wa kujifungua (CEmONC), awamu za utekelezaji ni tano, idadi ya vituo vya kutolea huduma vinavyopelekewa huduma ni 284. Huku jumla ya vifaa vilivyosambazwa hadi kufikia juni 2023 ni 299 sawa na asilimia 87.”
Tukai alieleza kuwa, “Utekelezaji wa mradi wa Uviko-19 unahusu hospitali na vituo vya vingine vya kutolea huduma za afya. Hospitali za Rufaa za Mikoa ambayo MSD Gharama za Mradi, ambapo thamani ya vifaa vinavyotarajia kusambazwa ni sh bilioni 99.7, thamani ya vilivyosambazwa ni sh bilioni 79.4. Asilimia za uekelezaji ni asilimia 80.”
Gharama za mradi huo, thamani ya vifaa vilivyotarajiwa kusambazwa ni Tsh bilioni 17.17 huku thamani ya vifaa vilivyosambazwa ni Tsh bilioni 17.62 sawa na asilimia 102 za utekelezaji.” alisisitiza Tukai na kusema MSD imefanikiwa kwenye ununuzi wa vifaa vya afya kwa kuanzisha kitengo cha Maalumu cha Usimamizi na Ufuatiliaji wa Mikataba.
“Ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani umeongezeka kutoka shil bilioni 14.1 mwaka wa fedha 2021/22hadi kufikia shil bilioni 39.77. kutoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi, zile ambazo zinakidhi mahitaji na viwango vya ubora hivyo kutegemea wazalishaji wa ndani.
“Kuanzisha zabuni malumu zinazohusu wazalishaji wa ndani hivyo kuongeza uwezo wa uzalishaji. Kuongeza idadi ya mikataba ya muda mrefu kutoka mikataba 100 yenye bidhaa za afya 711 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia mikataba 233 yenye bidhaa 2,209 kwa mwaka 2022/23.” alisisitiza Tukai.
Katika hatua nyingine MSD imebainisha mafanikio ya uzalushaji wa bidhaa za afya ambapo imekamilisha ujenzi wa kiwanda cha mipira ya mikono “gloves” kilichopo Idofi, Njombe. Kuhusisha sekta binafsi kwa kutambua maeneo ya uwekezaji wa bidhaa za afya za kimkakati za vidogo (tablets), rangi mbili (capusules), vimiminika na bidhaa zitokanazo na zao la pamba na kutangaza matamanio ya ushirikiano kati ya MSD na Sekta binafsi.
Pia MSD imekamilisha taratibu za usajili na uendeshaji za kiwanda cha barakoa cha N95 kilichopo Keko ambapo uzalishaji wake utakidhi mahitaji ya barakoa nchini sambamba na uanzishaji wa Kampuni tanzu “MSD Medipharma Manufacturing Company Ltd” itakayosimamia uzalishaji wa bidhaa za afya.”alisema Tukai.
Pamoja na mambo mengine, Tukai alieleza “Kuimarisha mfumo wa usambazaji kwa kusambaza bidhaa za afya mara 6 kwa mwaka (kila baada ya miezi miwili) kwa mwaka wa fedha 2022/23 badala ya mara nne kwa mwaka (miezi mitatu) hivyo kupunguza muda wa vituo vya afya kusubiri bidhaa za afya.
“Kununua matrela 16 yenye thamani ya Sh, bilioni 2.6 ili kuongeza kasi ya usambazaji wa bidhaa za afya, kuongeza usambazaji wa bidhaa za afya kwa asilimia 16 kutoka Sh, bilioni 320 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi Sh, bilioni 373 kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Kutumia mifumo ya shirikishi ya TEHAMA (PoD) ili kuhakikisha bidhaa za afya zinapokelewa kielektroniki katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuimarisha ufuatiliaji wa magari kwa kutumia mifumo.” alihitimisha Tukai.