Bohari ya Dawa Nchini – MSD, imeendelea kuongeza vifaa na bidhaa zinazohitajika kusaidia maafa yaliyotokea mkoani Manyara, kufuatia mafuriko yaliyotokea Desemba 3, 2023 ambayo yalisababisha vifo, kujeruhi, kuharibu mali na miundombinu.
Kuwasili kwa Majokofu hayo na Vifaa tiba, vilivyowasili hii leo Desemba 6, 2023 katika Hospitali ya Tumaini iliyopo Wilayani Hanang’ ni utekelezaji wa agizo la Serikali na kila moja lina uwezo wa kuhifadhi miili sita.
Hata hivyo, hatua hii ni muendelezo wa MSD wa kuwasilisha bidhaa za afya kwa ajili ya kusaidia maafa yaliyojitokeza katika wilaya ya hiyo Hanang.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson hii leo pia aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa uboreshaji wa huduma za afya, hali iliyosababisha majeruhi wote wa mafuriko ya Hanang kupata huduma Mkoani Manyara, bila kupewa rufaa.