Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassani Abbasi amesema wamepokea kwa masikito makubwa taarifa kuhusu ajali ya roli la mafuta iliyotokea Morogoro na kusababisha vifo vya watanzania zaidi ya 57 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa vibaya.

Dkt. Abbasi ameeleza kuwa Mkuu wa Mkoa na timu ya uokoaji wanaendelea kukabiliana na hali katika eneo la tukio.

“Tumepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu ajali ya lori la mafuta,  Morogoro, iliyosababisha moto na kuunguza watu kadhaa. Mkuu wa Mkoa na timu za uokoaji wanaendelea kukabiliana na  hali katika eneo la tukio. Taarifa kamili kuhusu idadi ya vifo na majeruhi itatolewa badae,” ameandika Dkt. Abbasi kwenye ukurasa wa Twitter.

Ameongeza kuwa “Tunaendelea kutoa wito kwa wananchi kukaa mbali na eneo la ajali hasa yanapohusika magari au vyombo vingine vya usafiri vilivyobeba vitu vinavyoweza kuripuka kama mafuta.”

Aidha lori hilo lililokuwa limebeba mafuta lilikuwa likitokea Dar es salaam na lilipofika Itigi, Morogoro likaanguka likiwa linamkwepa boda boda iliyokatiza mbele yake.

Watu mbalimbali wakiwemo waendesha bodaboda walifika katika eneo hilo la ajali kwa lengo la kuiba mafuta yaliyokuwa yakimwagika mara baada ya lori hilo kuanguka, moto ulilipuka na watu zaidi ya 57 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya na mlipuko huo.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema ajali hiyo imetokea mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi cha Msamvu ukitokea Dar es salaam.

 

JPM atuma salamu za rambirambi ajali ya Morogoro
Bilioni 4.6 kujenga chuo cha ufundi Karagwe