Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Betrice Singano amesema kampuni hiyo imekuja na promosheni ya kipekee’ Upige Mwingi na Airtel’ambapo mteja wa Airtel atajishindia zawadi ya muda wa maongezi papo hapo atapokuwa amefanya muamala wowote au kununua bando.

Ameyasema hayo leo Mei 3, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo ambapo amesema mteja muda wa maongeze na atajishindia zawadi ya fedha taslimu ya tsh milioni 50.

”Promosheni hii ni moja ya mfano wa jinsi tunavyoongeza thamani kwa kurudisha kwa wateja wetu na kuwaogezea hamasa ya kutumia huduma zetu bora kama Airtel Money kwa matumizi mbalimbali” amesema Singano.

Naye Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Andrew Rugamba amesema mipango ya Aitel ni kuendelea kusambaza huduma zake nchi nzima kwa kuendelea kupanua wigo wa mtandao wa Airtel.

Ameeleza kuwa mpaka sasa Airtel Money ina Branch zaidi ya 3,500 na wakala zaidi ya 200,000 huku wakiendelea kuwekeza kwenye kupanua mtandao wa 4G ili kufikia watanzania wote na hasa kwa maeneo ya vijijini.

”Sisi Airtel tunajali na tumejitolea kuhudumia wateja wetu, Airtel Tanzania ni kampuni ya kwanza kuondoa TOZO kwenye miamala ya simu kwa wateja wote na sasa ndiyo ya kwanza kuondoa gharama au makato ya kuangalia salio, hi inaongeza thamani sana kwa wateja kuokoa pesa na kukamilisha maana halisi ya kila mteja ni Airtel Money kuwa ni mshindi”amesema Rugamba.

Ufugaji wa kuhama unapunguza ubora bidhaa za mifugo - Majaliwa
Marc Guehi kumbadili Saliba Arsebal