Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambaye anawania muhula wa sita madarakani, amesema kwamba hajaona mtu mwenye uwezo wa kuongoza Uganda kwa sasa, na hivyo ataendelea kuwa madarakani kwa sababu wapiga kura nchini humo bado wanamhitaji kuendelea kuongoza taifa hilo.

Akihutubia viongozi wa chama chake cha National Resistance Movement (NRM) katika wilaya ya Lukungiri, ambayo ni ngome ya kisiasa ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu mara nne, Dk. Kiiza Besigye, Museveni amesema kwamba wapinzani wake ni watu wazembe wanaotaka kusukumwa kama mkokoteni.

Kati ya wapinzani wake 10 katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao 2021, ni waliokuwa makamanda muhimu wakati walipokuwa msituni katika vita vilivyomwezesha kuingia madarakani mwaka 1985.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani ajiuzulu
Wagombea hao ni, Lt. Gen Henry Tumukunde na aliyekuwa kamanda mkuu wa jeshi, Maj. Gen. Mugisha Muntu.

Dk. Besigye si mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, lakini anamfanyia kampeni mgombea wa chama chake cha Forum for Democratic Change, Patrick Amuriat.

Manya ala kiapo cha Ubunge, Unaibu Waziri

Besigye, Tumukunde na Muntu, wanaendelea kufanya kampeni katika sehemu kadhaa za Uganda wakimtaka Museveni kuondoka madarakani wakisema kwamba ameshindwa kutekeleza sababu kuu zilizowafanya kuingia msituni na kuanzisha vita vilivyomwezesha Museveni kuingia madarakani.

Lakini Museveni amesema kwamba wanaomkosoa walishindwa kazi licha ya kujaribu kila mara kuwaweka katika sehemu tofauti serikalini na sasa ‘wanampigia kelele.’

“Wanajua lengo langu katika siasa lakini wanataka kunishawishi niache msimamo wangu. Wanapiga kelele kwamba nastahili kuondoka madarakani utadhani sina pa kwenda,” amesema Museveni.


Bilionea Subash Patel afariki dunia
Biden athibitishwa rasmi na wajumbe

Comments

comments