Mahakama Kuu nchini Somaliland imemhukumu kwenda jela miaka mitatu msichana, Nacima Qorane anayeimba mashairi kwa kosa la kuhamasisha Somaliland kuungana na Somalia.

Somaliland ilijitenga na Somalia na kujitangazia uhuru wake mwaka 1991 licha ya kutotambuliwa umoja wa nchi za Kiafrika na kimataifa.

Aidha, Qorane alikamatwa mwezi Januari mwaka huu baada ya kurejea kutoka Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, alikokuwa akiimba mashairi ya kuhamasisha umoja.

Mwendesha mashtaka wa serikali amesema kuwa msichana huyo alikutwa na makosa ya uchochezi na kuitukana nchi yake ya Somaliland.

Hata hivyo, kituo cha haki za binadamu nchini Somaliland kimeiomba serikali ya nchi hiyo kumuachia huru Nacima Qorane na kuheshimu haki za binadamu.

 

Simba SC kuwakabili maafande wa jeshi la Magereza
Tanzia: Watu 7 wafariki dunia kufuatia mvua zinazonyesha Dar es salaam