Mshambualiaji wa Mtibwa Sugar, Charles Ilanfya amesema watahakikisha wanapambana vilivyo katika Michezo mitatu ya Ligi Kuu iliyosalia msimu huu 2022/23, ili kupata matokeo bora zaidi.

Mtibwa Sugar kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ipo nafasi ya 12, ikiwa na alama 29 baada ya kucheza michezo 27, huku ikibakiwa na michezo mitatu kumaliza msimu.

llanfya aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea KMC FC amesema tayari maandalizi yanaendelea kwa ajili ya michezo iliyosalia, na wachezaji wote wameonesha kuwa tayari kwa kusaka alama tisa za michezo hiyo.

“Tumeanza maandalizi kwa ajili ya michezo ijayo, tunafanya maandalizi ili kupata matokeo mazuri, tutapambana ili kufanya vizuri.”

“Kila mchezaji yupo tayari na tunajua kwamba ushindani ni mkubwa, hilo halitupi mashaka kwani tunajua ili kushinda lazima tushirikiane ndani ya uwanja,” amesema llafya

Mei 15 Mtibwa Sugar itacheza dhidi ya Polisi Tanzania itakayokuwa nyumbani mkoani Kilimanjaro katika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Mei 24 Mtibwa Sugar itakuwa nyumbani Manungu Complex mkoani Morogoro kwa kucheza dhidi ya Kagera Sugar.

Mei 28 itamaliza Ligi Kuu katika Uwanja wa nyumbani Manungu Complex kwa kuikribisha Geita Gold FC.

BMT yatoa wito kwa vyama, mashirikisho
Matukio Wachungaji tata: Yesu wa Kenya ajipeleka Polisi