Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, Geofrey Mwashiuya anatarajia kuachia ngazi katika kuitumikia timu ya Yanga na kwenda kulitumikia soka la nje ya nchi.
Amesema mpaka dakika hii kuna timu mbili nje ya nchi ambazo zimeonekana na nia ya kumsajili, nchi hizo ametaja kuwa ni Uingereza na Morocco.
Ambapo ametaja timu hizo kuwa ni pamoja na Tottenham Hostspur ya Uingereza.
Utaratibu wa kuhamia soka la nje utakamilika mara baada ya Mwashiuya kumaliza mkataba wake na timu ya Yanga, ikiwa amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake.
Kiungo huyo mshambuliaji kabla ya kusajiliwa na timu ya Yanga, alikuwa mchezaji wa Kimondo FC.
Na amekuwa na wakati mgumu wa kuanza kikosi cha kwanza lakini amevumilia.