Rais Trump anakabiriwa na wakati mgumu wa kufanya tathmini juu ya mazingira ya mshauri wake Generali Michael Flynn, baada ya kugundulika kuwa alifanya  mazungumzo na balozi wa Urusi kuhusiana na vikwazo dhidi ya Marekani muda mfupi kabla ya Raisi Trump hajachukua hatamu za madaraka.

Bi Nancy Pelosi,  kiongozi wa chama cha Demokratic amtaka Rais wa Marekani Donald Trump kumfukuza kazi mshauri wake Michael Fynn, na kusema kwamba generali Michael Fynn anaweza kuwa si mtu wa kumuamini, anaweza kuweka maslahi ya Marekani nyuma na kuweka maanani maslahi ya Urusi  kwamba baadae anaweza kuudanganya umma wa wamerekani juu ya mawasiliano yake.

Imefahamika pia kuhusiana na mawasiliano yake na shirika la upelelezi la Marekani FBI na uchunguzi wake juu ya uhusiano wa raisi Trump na raisi wa Urusi , Vladimir Putin.

Marekani

Man City Yaunguruma England
Video: Sakata la dawa lageukia majaji, Mke mume jela miaka 20