Maafisa wa polisi nchini New Zealand wamempiga risasi na kumuua mtu mwenye itikadi kali aliyezua vurugu baada ya kuwachoma kisu na kuwajeruhi watu sita katika duka moja la mjini Auckland Newzealand.
Waziri mkuu Jacinda Ardern amesema kwamba tukio hilo lilikuwa shambulio la kigaidi lililotekelezwa na raia mmoja wa Sri Lanka ambaye alikuwa akichunguzwa na polisi.
Ardern amesikitishwa na kitendo hicho kwa kusema kile kilichotokea kilikuwa kitendo cha chuki kwa sababu kilitekelezwa na mtu binafsi sio dini.
Kati ya watu sita waliojeruhiwa , watatu ni mahututi na mmoja akiwa katika hali mbaya, kwa mujibu wa maafisa wa Afya.
Shambulio hilo lilifanyika katika duka la jumla la Lynn Mall katika wilaya ya New Lynn na Mshambuliaji alidaiwa kuchukua kisu kikubwa kutoka katika rafu ya duka na kuanza kuwachoma kisu watu waliokuwa karibu naye .