Polisi jijini London nchini Uingereza walilazimika kufika katika hotel aliyofikia Justin Bieber baada ya kupata taarifa za msichana mmoja aliyeenda kula bata na mwimbaji huyo kugeuka mwehu.

Kwa mujibu wa ‘The Sun’, Polisi walifika katika hotel aliyofikia Bieber majira ya saa kumi na mbili alfajiri.

Inaelezwa kuwa usiku wa kuamkia siku hiyo mwimbaji huyo aliingia hotelini hapo akiwa na wasichana kadhaa akitokea nao kwenye kumbi za starehe. Lakini mmoja kati ya wasichana hao aligeuka na kuanza kupiga mayowe akiwa peku katika eneo la mapokezi.

“Rafiki zangu wako wapi!? Naita polisi,” anadaiwa kulia mrembo huyo.

Uongozi wa hotel hiyo ulilazimika kuita polisi kumaliza sakata hilo kwa amani.

Polisi walitoa tamko lao baadaye na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo na wao kufika na kutoa msaada. Hata hivyo, walieleza kuwa msichana huyo alikuwa salama na kwamba hakuna makosa yoyote yaliyofanywa dhidi yake.

 

Azam FC Watekeleza Agizo La Rais John Magufuli
Wananchi Kuamua Ukomo wa Urais wa Kagame Mwezi Huu