Mkuu wa SMAUJATA, Idara ya wanafunzi Vyuo na Vyuo Vikuu Taifa, Irene Mashine amewataka wanafunzi wa vyuo kutoa fumbia macho vitendo vya ukatili wa ikiwemo usafirishaji haramu wa binadamu na ngono wawapo vyuoni.
Irene ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini – TUDARCO, katika semina iliyolega kutoa elimu kwa kundi hilo namna ya kupambana na changamoto hizo hasa biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Amesema, wanafunzi wa vyuo vingi wamekua wakifanyiwa ukatili lakini wamekua wakinyamaza na kushindwa kuzungumaza kwa watu jambo ambalo lina waathiri kisaikolojia katika masomo na wengine wamekua wakiombwa rushwa ikiwemo ya ngono na pesa, jambo hilo halipaswi kuzoeleka wala kufumbiwa macho kwani linaharibu dhima ya utu wao.
Aidha, Irene amewataka wanachuo hao kutambua nafasi zao ni kwanini wapo chuoni na wana malengo gani, ili watimize majukumu yao pamoja na kuachana na tamaduni za watu wengine ambazo zipo nje ya utu na utamaduni wa kitanzania.
Hata hivyo, amesema wanachuo wanatakiwa kutambua aina za ukatili na namna ya kukabiliana nazo ambapo amesema Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima waliagiza kuanzishwa kwa madawati ya jinsia vyuoni, ili kupambana na changamoto za vitendo vya ukatili.